Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally
Hapi ametangaza na kutoa agizo kwa viongozi wa Halmshauri ya Kinondoni
kuanza kutoa mikopo ya vitendea kazi kwa vijana mbalimbali wilayani huo
zikiwemo Pikipiki ili vijana waweze kujikwamua kiuchumi.
Ali
Hapi amesema hayo alipowatembelea Wafanyabiashara wa soko la ndizi
ambao wanategemewa kuhamishwa katika eneo la Kigogo Dampo siku za
karibuni na kudai kuwa zipo fedha zaidi ya Bilioni 1 kwa ajili ya mikopo
kwa vikundi vya vijana na kina mama ambazo zimekuwa hazitoki kwa kuwa
watu wamekuwa hawataki kijiunga katika vikundi na kwenda kukopa.
"Vijana wanaotaka kukopa Pikipiki waje, waje wajiorodheshe wakopeshwe Pikipiki walete rejesho serikalini tuna Billioni 1 imekaa tuu pale eti tunasubiri vijana waje, watakuja lini? Sasa nataka kuona vijana wananufaika na fedha hizo wajikwamue ili familia zao nazo zinufaike" Alisema Hapi

Mkuu wa Wilaya aliendelea kusisitiza kuwa "Nataka tuwakopeshe watu vitu ambavyo vinawasaidia
moja kwa moja, tunataka tuwakopeshe watu dhana za kufanyia kazi nimeshaanza kumwambia Mkurugenzi jambo hilo walifanye. Naibu Meya wakijitokeza vijana 400 Kinondoni tukawakopesha Pikipiki nataka nikuakikishie ndani ya muda mfupi fedha zile zinarudi, mpe mtu Pikipiki chukua kadi itunze yeye analeta marejesho kila wiki unauhakika hapo"

Comments
Post a Comment